Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yildirim ametaka kuondolewa madarakani kwa Rais wa Syria Bashar al-Assad.
Yildirim anaishutumu serikali ya Assad kwa kutengeneza mazingira yanayoipa nguvu kundi la wanamgambo wa IS.
Ameongeza kuwa kwa kipindi hiki ambacho Assad anaendelea kutawala nchini Syria,tatizo la IS kamwe halitatatulika.
Akihojiwa na BBC Yildirim amekanusha uvumi kuwa Uturuki italegeza msimamo wake na kumuunga mkono Assad.
Post a Comment