Mahakama nchini Zimbabwe imemuachilia huru Mchungaji aliyeongoza kampeni mitandao dhidi ya usimamizi mbaya wa serikali.
Akitupilia mbali kesi hiyo, hakimu wa mahakama hiyo amesema waendesha mashtaka wamebadili mashtaka yanayoimkabili Mchungaji Evan Mawarire bila ya kumjulisha. Mamia ya wafuasi wake walishangilia uamuzi huo ulipotolewa.
Awali waendesha mashtaka walimshtaki kwa kuchochea ghasia wakati alipokamatwa siku ya Jumanne, lakini baadaye walimlaumu kwa jaribio la kutaka kuipindua serikali.
Katika kampeni zake hizo, Mchungaji Mawarire aliwahimiza Wazimbabwe kupitia mitandao ya kijamii kupambana na vitendo vya rushwa pamoja na ukosefu wa ajira.
Post a Comment