0
Aliyekuwa mpenzi wa zamani wa mwanamuziki nguli wa RnB and PoP nchini Marekani Mariah Carey, Nick Cannon, sasa amenyakuwa kitu kipya katika mahusiano na kuweka wazi kuwa wako pamoja na wanafurahia maisha mapya katika siku za usoni.
Cannon (35) ameingia kwenye “Headlines” za vichwa vya Habari nchini Marekani mara baada ya kuonekana akijivinjari katika kumbi mbali mbali za Starehe pamoja na Fukwe za Bahari nchini humo pamoja na Mwanamuziki wa Kundi la TLC Rozanda “Chill” Thomas kwa kipindi cha hivi karibuni.
Mshereheshaji huyo wa kipindi cha Runinga cha America`s Got Talent alibwagwa na Maria Carey (47) ambaye wameishi nae kwa takriban miaka 8 mara baada ya kuwa na matatizo ya kila mara katika ndoa yao ikiwemo kuruka viwanja na wanawake wengine pamoja na matumizi mabaya ya kifedha ambayo alikuwa wakiingiza kwa pamoja.
Rozanda “Chill” Thomas (45) alikuwa mmoja wa washiriki wa kundi la TLC TANGU 1991 na aliwahi kupata ujauzito akiwa na umri wa miaka 20 kutoka kwa producer Dallas Austin lakini mimba hiyo kuharibika kutokana matunzo mabovu lakini waliendelea na Mahusiano na kufanikiwa kushika mimba nyingine na kupata mtoto wa Kiume aliyeitwa Tron Austin mwaka 1997.
Thomas pia aliwahi kutoka kimahusiano na Usher Raymond 2001 lakini mahusiano yao hayakudumu na kuvunjika mara baaya ya miaka miwili tu 2003.
Kwa sasa Maria Carey anatoka kimahusiano na Bilionear James Packer ambaye amekwisha mvalisha pete ya Uchumbo mwanamama huyo aliyezaa watoto wawili pamoja na Nick Cannon.

Post a Comment

 
Top