0
Waziri mkuu mpya wa Uingereza Bi Theresa May amewashangaza wengi kwa kumteua Boris Johnson kuwa waziri anayeshughulikia masuala ya kigeni.
Johnson ambaye ni Meya wa zamani wa London,alikuwa mmoja wa wahamasishaji wakuwa wa Uingereza kujitenga na umoja wa Ulaya.
Baada ya Uingereza kujitoa ndani ya umoja huo akatajwa kama mmoja wa watu wanaopewa nafasi kubwa kuwa waziri mkuu.
Waziri wa zamani wa amasuala ya kigeni Philip Hammond,ameteuliwa kuwa waziri wa fedha.

Post a Comment

 
Top