0
Brazil itatoa fedha za ziada, dola milioni 24 kwa ajili ya jeshi kuimarisha ulinzi kuelekea mashindano ya Olympiki, Rio de Janeiro
Waziri wa Michezo Leonardo Picciani amesema jeshi litaanza kufanya doria viwanjani kuanzia Julai 24.
Michezo hiyo ya Olympiki inatarajiwa kuanza mwezi ujao.
Zaidi ya Polisi elfu 80 na wanajeshi watafanya doria katika mitaa ya mji wa Rio katika kipindi hicho cha michezo.
Polisi mjini humo katika siku za hivi karibuni polisi walifanya mgomo dhidi ya kuchelewa kwao kulipwa mishahara na ukosefu wa mahitaji mengine muhimu kama vile mafuta ya gari.

Post a Comment

 
Top