0
Klabu ya Sunderland imetoa ruhusa kwa chama cha soka nchini Uingereza FA kuzungumza na meneja wake Sam Allardyce kuhusu mpango wa kuinoa timu ya taifa ya England.
Lakini wakati huohuo timu hiyo inayoshiriki ligi kuu imesema kuwa inatamani meneja wake huyo asalie katika klabu yake kwani ana umuhimu mkubwa.
Sunderland inadai tetesi za Allardyce kuwa kocha wa timu ya taifa zinamfanya ashindwe kutulia na kuwa na mipango mipya ya klabu kwa msimu ujao.
England inasaka meneja mpya baada ya Roy Hodgson kubwaga manyanga June 28.
Alijiuzulu baada ya England kutolewa na Iceland katika hatua ya 16.

Post a Comment

 
Top