0
Urusi inasema kuwa Rais Erdogan wa Uturuki ameomba msamaha kwa hatua ya taifa lake, kuidungua ndege ya kivita ya Urusi karibu na mpaka na Syria mwaka jana.
Katika ujumbe ulioandikwa ndani ya barua hadi Kremlin kwa Rais Putin, Bwana Erdogan alielezea masikitiko yake makubwa kwa kile kilichofanyika, huku akisema anataka kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili.
Image copyrightREUTERS
Image captionNdege ya Urusi iliyodunguliwa
Uturuki bado haijatoa maelezo kuhusiana na barua hiyo.
Udunguaji wa ndege hiyo uliibua mgongano mkubwa wa kisiasa, uliopeleekea Urusi kuiwekea Uturuki vikwazo vya kibiashara ambavyo vingeondolewa tu baada ya Rais Erdogan kuomba msamaha.

Post a Comment

 
Top