0
Idadi ya watu waliokufa wakati wa shambulio la kigaidi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ataturk uliopo mji wa Instanbul, Uturuki imefikia 41 na wengine 239 kujeruhiwa.
Maafisa wa nchi hiyo walisema washambuliaji watatu walianza kufyatua risasi ndani na nje ya uwanja huo kabla ya kujilipua kwa mabomu baada ya polisi kuwafyatulia risasi.
Waziri Mkuu wa Uturuki, Binali Yildirim alisema dalili za mwanzo zilionyesha kikundi cha Islamic State kilihusika lakini hakuna aliyekiri kushambulia.
Kikundi cha Islamic State na waasi wa Kikurdi walihusishwa katika mashambulio ya kigaidi ya hivi karibuni nchini Uturuki.
Rais wa Tayyip Erdogan wa Uturuki alisema shambulio hilo linapaswa kubadili mwelekeo katika vita dhidi ya ugaidi na makundi ya wanamgambo duniani.
"Mabomu yaliyolipuka mjini Istanbul yangeweza kulipuka uwanja wowote wa ndege katika mji wowote ule duniani," alisema.
Taarifa ya serikali ya Marekani imeliita shambulio hilo uhaini ikisema nchi hiyo inabaki imara katika kuiunga mkono Uturuki.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Thomas de Maiziere aliliita shambulio hilo kuwa ni kitendo cha uoga na kikatili.

Post a Comment

 
Top