Idadi ya watu waliofariki kufikia sasa Nchini Indonesia imepata na kufikia saba.
Watu hao wamefariki na wengine kadhaa kupata majeraha mabaya baada ya kuchomwa na gesi iliyochangamana na moshi wa volkeno baada ya mlima mmoja kulipuka magharibi mwa nchi hiyo.
Habari zaidi zinasema kuwa majivu imerushwa angani huku tope la volkeno likitapakaa kilomita tatu na kusababisha vifo vya watu hao.
Waathiriwa wote waliofariki walikuwa shambani wakilima katika eneo ambalo lilitangazwa na wakuu wa Indonesia kama maeneo hatari kwa kuwa karibu mno na mlima wa volkeno wa Sinabung.
Makundi ya uokoaji yamefika maeneo hayo ili kuwahamisha watu na kutafuta manusura au maiti zaidi ya waliofariki.
Post a Comment