Jeshi la Nigeria limesema kuwa msichana mwingine aliyetekwa na wanamgambo wa Boko Haram zaidi ya miaka miwili iliyopita kutoka shule ya Chibok ameokolewa.
Msemaji wa Jeshi kanal S K Usman hakueleza kwa undani namna ambayo msichana huyo ambayr hakutajwa jina aliokolewa,lakini akasema patakuwa na maelezo zaidi baadae.
Siku ya Alhamisi msichana mwingine mwenye miaka 19 ambaye alifnikiwa kutoroka katika kambi ya Boko Haram, Amina Ali Nkeki,alipelekwa katika mji mkuu Abuja akiwa na mtoto wake alizaliwa wakati ametekwa, kwa ajili ya kukutana na Rais wa nchi hiyo Muhammadu Buhari.
Zaidi ya wasichana wengine mia mbili bado hawajapatikana,huku ikidhaniwa kuwa bado wanashikiliwa katika misitu ya Sambisa karibia na mpaka wa Cameroon.Gavana wa jimbo la Borno amesema kwamba jeshi la nchi hiyo limejiandaa kuwakomboa wasichana hao.
Post a Comment