Zoezi la kutafuta mabaki ya ndege ya Misri iliyopotea hapo jana, leo limeingia siku ya pili ambapo tayari serikali ya Misri imesema ndege hiyo inawezekana ikawa imetunguliwa na magaidi na sio tatizo la kiufundi.
Nayo serikali ya Ufaransa inasema inajaribu kuchunguza iwapo taratibu za usalama hazikufuatwa huko mjini Paris. Maafisa usalama waliokuwa zamu wakati ndege hiyo Egypt air ilipopaa kuelekea Cairo wameanza kuhojiwa.
Ndege hiyo iliyokuwa na abiria sitini na sita ilipotea ilipokuwa njiani kutokea Ufaransa kuelekea mji mkuu wa Misri Cairo.
Wataalamu wa masuala ya usalama wanasema kama kulikuwa bomu kwenye ndege hiyo ingetua mara kwa mara.
Kabla ya kufika Paris ufaransa ndege hiyo ilitua katika miji ya Cairo, Tunis na Eritrea. Usalama katika uwanja wa ndege umeimarishwa tangu tukio la ugaidi lililotokea mwaka jana.
Nayo Serikali ya Misri imesema ndege hiyo ina uwezekano mkubwa kuwa ilitunguliwa na magaidi na si tatizo la kiufundi.
Maafisa usalama na ufundi kutoka Ufaransa wamekwenda Cairo nchini Misri kusaidiana na mamlaka ya nchi hio kwa ajilli ya kufanya uchunguzi.
Bado kumekuwa na sintofahamu kuhusu eneo la mwisho ndege hiyo MS804 ilipopotelea takriban nusu saa kabla ya kutua.
Zoezi la kuitafuta ndege hiyo na mabaki yake bado linaendelea karibu na kisiwa cha Ugiriki cha Karpathos.
Tayari uchunguzi umeanza ambapo ulinzi mkali umeimarishwa katika uwanja wa ndege Charles de galles huko Paris Ufaransa.
Post a Comment