Mamlaka ya kuzuia majanga katika jimbo la Bihar nchini India imewashauri wakaazi wa eneo hilo kutopika kati ya saa tatu asubuhi na saa 12 ili kuzuia kuzuka kwa moto wakati huu wa msimu wa joto.
Wakaazi wameshauriwa kutofanya matambiko ya kuwasha moto ama hata kuchoma mimea ilionyauka na jua.
Ushauri huo ulitolewa siku ya Jumatatu kutokana na agizo kwa waziri mkuu.
Hatua hiyo inajairi baada ya ripoti kwamba watu 67 walifariki katika visa vya moto katika jimbo hilo katika kipindi cha mwezi uliopita. Maneo kadhaa ya India ,ikiwemo Bihar yanakumbwa na mawimbi ya joto huku vipimo vya joto vikifikia 40C.
Baada ya kuangazia visa vya moto tulibaini kwamba vyote vilisababishwa na moto wa kupikia.
Hii ndio maanatumetoa ushauri kwa wana vijiji kwamba wamalize kupika kabla ya saa tatu asubuhi na kuzima moto ,alisema afisa mkuu anayesimamia mamlaka hiyo ya majanga.
Post a Comment