0
Maafisa wa kijeshi wa Korea kusini wanasema Korea kaskazini imefyatua kombora hilo kutoka Wonsan, eneo lililo kambi ya jeshi mashariki mwa pwani ya Korea Kaskazini.
Inaamika kuwa jaribio hilo lilikuwa la pili la makombora ya Korea kaskazini la masafa ya wastani inayojulikana kama Musudan, ambayo yana uwezo wa kufika katika vituo vya kijeshi vya Marekani vilivyoko katika kisiwa cha Guam katika bahari ya Pasifiki.
Lakini utawala wa Pyongyang hauna nguvu kwa sasa ya kutumia makombora hayo.
Jaribio jingine la makombora hayo mwezi uliopita, halikufanikiwa baada ya kombora hilo kulipuka muda mfupi baada ya kurushwa.
Kumekuwa na wasi wasi kuwa utawala wa Pyongyang umekuwa ukiimarisha uundaji wa zana zake za nyuklia, kabla ya kufanyika kwa kongamano kuu la chama tawala mwezi ujao.
Image captionKim Jong Un wa Korea kaskazini
Mkutano huo unadhamiria kuonyesha mamlaka ya kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un.
Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye, ameonya kuwa korea Kaskazini itawekwa vikwazo zaidi ikiwa itaendeleza majaribio hayo.
'Ikiwa korea kaskazini itaendelea na majaribio zaidi ya nuklia, itakuwa inafanya uchochezi na kukiuka sheria za kimataifa kama ilivyoidhinishwa na azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa tangu ilipofanya jaribio lake la nne. Tutakumbwa na hali tofauti sana kuliko ilivyo sasa, kwa sababu korea kaskazini imekuwa ikifanya majaribio hayo kwa muda wa miaka mitatu'.
Vikwazo zaidi vya kimataifa viliwekea kora kaskazini baada ya majaribio hayo ya makombora ya masafara marefu ya nuklia mwaka uliopita.

Post a Comment

 
Top