Msikiti uliokuwa ukikarabatiwa umeporomoka nchini Somalia na kuwaua watu 15 na kuwajeruhi wengine 40.
Kisa hicho kilitokea katika msikiti mmoja wa mjini Mogadishu wakati wa ibada ya Ijumaa.
Hatahivyo maelezo yalitolewa siku ya Jumamosi.Mamia ya watu walidaiwa kuwa ndani ya msikiti huo wakati ulipoporomoka na wengine wanaaminika kuwa chini ya vifusi vya jengo hilo la ibada.
Muhandisi mmoja aliyekuwa akiufanyia ukarabati misikiti huo alikamatwa kwa tuhuma za uzembe,vyombo vya habari vya eneo hilo vimeripoti.Mvua kubwa imenyesha katika eneo hilo katika siku chache zilizopita.
Serikali ya Somalia inadhibiti Mogadishu na miji mingine,lakini wapiganaji wa al-Qaeda wanaoshirikiana na kundi la wapiganaji wa al-Shabab wanatawala maeneo mengi ya mashambani.
Zaidi ya wanajeshi 22,000 wa Umoja wa Afrika na polisi wamepelekwa nchini humo kuilinda serikali
Post a Comment