Maafisa wakuu nchini Marekani wanasema kuwa Rais Barack Obama atatuma wanajeshi ya ziada wapatao 250 nchini Syria, ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na vikosi vya ndani vya nchi hiyo, katika kupambana na wapiganaji wa Islamic State.
Kwa mujibu hao wa maafisa wa Marekani, lengo hasa ni kuwasajili waarabu wa dhehebu la Sunni kuungana na wapiganaji wa kikurdi waliopo kaskazini mashariki mwa Syria.
Hata hivyo vikosi hivyo vya Marekani havitawajibika moja kwa moja katika mapambano hayo.
2. Jopo lasema serikali Mexico ilitatiza uchunguzi
Jopo la wataalamu wa kimataifa wanaochunguza kupotea kwa walimu wakurufunzi wapatao 43 mnamo mwaka 2014, linasema kuwa serikali ilitatiza uchunguzi huo.
Wataalamu hao wanapuuzilia mbali taarifa ya mwisho kwamba waalimu hao walipeanwa kwa genge la majambazi na maafisa wafisadi wa polisi.
Inasemekana kuwa genge hilo liliteketeza miili ya wanafunzi hao katika eneo la utupaji taka.
3. Mvulana wa miaka 16 ashtakiwa ugaidi Australia
Polisi nchini Australia wamemshtaki mvulana mwenye umri wa miaka 16, ambaye anasemekana alikuwa akipanga kutekeleza shambulio katika siku kuu ya wanajeshi wastaafu wa nchi hiyo.
Mvulana huyo alitiwa mbaroni nyumbani kwake huko Sydney, alipodaiwa kupanga kutekeleza uhalifu huo wa kigaidi leo Jumatatu wakati wa sherehe za siku kuu ya ANZAC, ya maadhimisho hayo ya kuwakumbuka wanajeshi waliouawa vitani Australia.
4. Chama tawala chashinda uchaguzi Serbia
Chama tawala cha Progressive nchini Serbia, kimepata ushindi mkubwa katika matokeo ya kura ya ubunge, huku nusu ya kura zote zikiwa zimehesabiwa.
Matokeo hayo yameonekana uidhinishaji wa sera za waziri mkuu Aleksandar Vuchich za kuunga mkono Umoja wa Ulaya (EU).
5. Sisi asihi raia Misri wakatae maandamano
Na Rais wa Misri, Abdul Fattah al-Sisi, amewaomba raia wa taifa hilo kulinda taifa, kabla ya kufanyika kwa maandamano makubwa ya kuipinga serikali ya nchi hiyo, baadaye leo Jumatatu.
Bw Sisi anasema kuwa jitihada za kuyumbisha amani nchini Misri, hazitafua dafu, ikiwa tu raia wa taifa hilo watasimama kidete.
Uhasama dhidi ya serikali umeongezeka majuzi baada ya utawala wa nchi hiyo kuipa Saudi Arabia visiwa viwili vilivyoko katika eneo la Bahari ya Sham
Post a Comment