0
Rais Obama ameanza ziara rasmi Ujerumani, akiwa na lengo la kuzungumzia mkataba wa kibiashara unaopendekezwa, baina ya Marekani na bara la Ulaya, uitwao T-TIP.
Kabla ya ziara yake, Waziri wa uchumi wa Ujerumani, Sigmar Gabriel, aliliambia gazeti la Handelsblatt, kwamba WaMarekani hawataki kampuni za Ulaya kuomba kandarasi za Marekani.
Hapo jana, maelfu ya watu waliandamana, katika mji wa Hanover, kupinga mkataba huo.
Rais Obama atakuwa mjini humo kwa siku mbili zijazo.
Rais Obama anasema mkataba huo utaleta ajira na kukuza uchumi.
Lakini muandishi wa BBC mjini Berlin, anasema atakuwa na kazi pevu ya kushawishi watu wakubaliane naye.

Post a Comment

 
Top