Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Haki za Kibinadamu ameshutumu sera za mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani, akisema ni sawa na ushenzi.
Zeid Raad al-Hussein, ingawa hakumtaja Bw Trump moja kwa moja, alizungumzia hatua ya mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York kuunga mkono mateso pamoja na sera zake kali dhidi ya Waislamu.
“Ushenzi na ulokole si thibitisho la uongozi thabiti,” Hussein alisema.
Kamishna huyo pia amekosoa mpango wa mgombea mwengine Ted Cruz wa kuweka mpango wa kupeleleza maeneo wanamoishi Waislamu.
“Kutoa matamshi ya chuki, kuchochea na kuwatenga wengine si jambo la kuburudisha watu nalo, au jambo la kujifaidi kisiasa,” Bw Hussein ameambia hadhira katika mji wa Cleveland, Ohio.
Ameongeza: "Mmoja wa wagombea wanaoongoza katika kinyang’anyiro cha kutaka kuwa rais wa nchi hii alitangaza, miezi kadha iliyopita, kujitolea kwake kutumia mateso (…) kuumiza watu wengine, ili watoe habari au wabuni habari ambazo hawazo nazo.Wakati wa kampeni, bw Trump alisema kwamba mateso wakati mwingine hufanikiwa na akaahidi kurejesha njia hatari zaidi kuliko kutumia maji kulazimisha washukiwa kufichua habari.
Njia hizo zilitumiwa na jeshi la Marekani katika washukiwa wa ugaidi lakini zilipigwa marufuku na utawala wa Bw Obama.”
Post a Comment