Huku mgogoro wa kisiasa ukizidi kuota mizizi nchini Iraq, spika wa bunge la nchi hiyo,Salim al-Jabouri amechukua mamuzi ya kuahirisha kikao cha bunge hilo kwa sababu za kiusalama .
Ingawa baadhi ya wabunge wa bunge hilo wameamua kuendelea na kikao hicho kwa namna ya yoyote bila ya kuwa na spika huyo na badala yake watachagua spika mpya.
Kati kati ya sintofahamu hiyo kuna mpango wa waziri mkuu wa nchi hiyo Haider al-Abadi kupambana na rushwa , akiwa na mpango wa kufuatilia nyendo za baadhi ya wabunge wa bunge hilo na watendaji wengine wa serikali yake.
Nchini Iraq kuna hisia miongoni mwa wabunge imekuwa haraka mno huku kikao cha bunge hilo siku chache zilizopita kumalizika kwa mapambano ya nguni miongoni mwa wabunge .
Post a Comment