0
Mchezaji chipukizi wa Kriketi raia wa Uingereza amefariki baada ya kuripotiwa kupigwa risasi na majambazi nchini Trinidad.
Adrian St John , mwenye umri wa miaka 22 ambaye alikichezea chuo cha mafunzo cha Chris Gayle mjini London anaaminika kufariki siku ya Jumapili.
Mchezaji wa kriketi wa West Indies Gayle alichapisha ujumbe kwenye mtandao wa Twitter akisema " Ni habari mbaya kusikia ,Rambirambi zangu kwa familia na marafiki." Adrian St. John alikuwa nahodha katika chuo hicho.Ofisi ya maswala ya mambo ya nchi za kigeni imesema walikuwa kwney mazugumzo na maafisa nchini Trinidad kufuatia kifo cha raia huyo wa Uingereza.
Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kwamba Bwana St.John, alivamiwa baada ya kusimamisha gari lake ili kuwachukuwa rafiki zake alipovamiwa na kupigwa risasi.

Post a Comment

 
Top