0
 Timu ya soka ya Manchester city imefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya Michuano ya klabu bingwa barani ulaya baada ya kuwafunga Psg ya Ufaransa jumla ya bao 1-0.
Wakicheza katika dimba lao la Etihad Manchester city walifanikiwa kuandika bao pekee na la ushindi Dakika ya 76 kipindi cha pili kupitia kwa mchezaji De Bruyne.
Kwa ushindi huo Manchester city wameifunga Psg jumla ya mabao 3-2 baada ya timu hizo kufungana bao 2-2 katika mchezo wa awali.
Kwingineko Real Madrid imeichapa Wolf-Sburg 3-0 kupitia mabao ya mchezaji Christiano Rolnado ikiwa ni Hat trick yake katika mchezo huo.
Katika mchezo wa awali Wolf-Sburg walishinda 2-0 hivyo Real Madrid wamesonga mbele katika hatua ya Nusu fainali.
Michuano hii inaendelea tena Jumatano kwa michezo miwili, Benfica itamenyana na Bayern Munich huku Atletico Madrid ikichuana na Barcelona katika dimba la Bernabeu.

Post a Comment

 
Top