Marekani itatuma majeshi ya ziada 250 kuunga mkono jitihada zinazofanywa na vikosi vya ndani vya nchi hiyo IS.
Kwa mujibu wa maafisa wa Marekani, lengo hasa ni kuwashajiisha waarabu wa dhehebu la sunni kuungana na wapiganaji wa kikurdi waliopo kaskazini mashariki mwa Syria.
Vikosi vya Marekani havitawajibika katika mapambano.
Kupelekwa kwa vikosi hivyo kutafanya idadi ya vikosi vya Marekani vilivyopo nchini Syria kufikia mia tatu.
Mwanzoni, Chancellor wa Ujerumani, Angela Merkel, amezitaka pande zinazohasimiana nchini Syria kutenga eneo salama ambalo wakimbizi wanaokimbia vita wanaweza kulindwa ndani ya nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na rais Obama, Merkel amesema ni matumaini yake kwamba mpango huo hatimae unaweza kuridhiwa katika mazungumzo ya amani yatakayofanyika Geneva:
Kwa upande wake, rais Obama amesema itakuwa taabu sana kuwepo kwa njia salama ambayo itakuwa inalindwa na vikosi vya kigeni pekee:
Lakini wakati huo huo akaongeza kusema kuwa mpango uliopendekezwa na Angela Merkel unaweza kufanya kazi iwapo pande zote zinazopigana zitaukubali
Post a Comment