Kundi la wapiganaji wa Islamic State limetangaza kuwa kwamba tawi lake la Afrika magharibi la Boko Haram lina kiongozi mpya.
Abu Musab al-Barnawi ambaye alikuwa msemaji wa kundi hilo ndio anayeonekana kuchukua uongozi wa kundi hilo.Hatahivyo kundi halijasema nini kilichomtokea aliyekuwa kiongozi wake Abubakr Shekau.
Mara ya mwisho kusikika ni katika kanda ya sauti mwezi Agosti akisema kuwa yuko hai na kwamba nafasi yake haijachukuliwa -huku kanda ya video ya ISIS iliotolewa mwezi Aprili ikithibitisha hilo.KUndi la Boko Haram ambalo limepoteza eneo kubwa lililokuwa likidhibiti miezi 18 iliopita linapigana kuiondoa madarakani serikali ya NIgeria.
Mashambulio yake ya miaka saba yamesababisha vifo vya watu 20,000 hususan katika eneo la Kaskazini mashariki
Post a Comment