0
Tai mmoja mkubwa nusura afanye kitendo cha kustaajabisha ,,, tai huyo alijaribu kumtwaa mvulana mmoja na kupaa naye nchini Australia!
Umati wa watu uliokuwa katika hifadhi ya Alice Springs Desert Park ulipigwa na butwaa tai huyo alipojaribu kumbeba mtoto wakati wa kurekodi kwa onyesho moja la wanyama pori.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa ''ilikuwa ni kama tai huyo aliona mnyama mdogo ambaye alitaka kumfanya mlo wake''
Image copyrightCHRISTINE OCONNELL INSTAGRAM 55CHRIS
Image captionWalioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa ''ilikuwa ni kama tai huyo aliona mnyama mdogo ambaye alitaka kumfanya mlo wake''
Mvulana huyo anayekisiwa kuwa kati ya miaka 6-8 aliepuka kwa kupiga kamsa na mwishowe ndege huyo mkubwa akapaa na kutoweka.
Mvulana huyo alitibiwa baada ya makucha ya ndege huyo kumgwara usoni.
Image copyrightCHRISTINE OCONNELL INSTAGRAM 55CHRIS
Image captionHata hivyo wahudumu wa hifadhi hiyo waliingilia kati na kumfukuza tai huyo.
Bi Christine O'Connell kutoka Horsham katika jimbo la Victoria aliyenasa tukio hilo kwa kamera anasema tai huyo alimvamia mtoto huyo akijaribu kumuinua.
Hata hivyo wahudumu wa hifadhi hiyo waliingilia kati na kumfukuza tai huyo.
Image copyrightCHRISTINE OCONNELL INSTAGRAM 55CHRIS
Image captionWasimamizi wa hifadhi hiyo wamemuondoa tai huyo kwenye onyesho hilo.
Waandalizi wa onyesho hilo walifungasha virago vyao kwa haraka baada ya tukio hilo maarufu.
Wasimamizi wa hifadhi hiyo wamemuondoa tai huyo kwenye onyesho hilo.

Post a Comment

 
Top