0
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dkt Kizza Besigye, ambaye amezuiliwa kwa wiki kadha, ameachiliwa huru kwa dhamana na Mahakama Kuu nchini humo.
Jaji Wilson Masalu Musene amempa kiongozi huyo wa chama cha Forum for Democratic Change dhamana ya dola 30,000 za Marekani.
Jaji amemwamuru Dkt Besigye kutojihusisha na vitendo vya kuzua ghasia na adumishe amani katika jamii hadi kesi ya uhaini inayomkabili isikizwe na uamuzi kutolewa.
Ametakiwa awe akifika kortini mara moja kila wiki mbili kuanzia Julai 26.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, wafuasi wa Beisgye wameimba wimbo wa taifa wa Uganda na kushangilia baada ya kiongozi wao kupewa dhamana.

Post a Comment

 
Top