Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Malala Yousafzai amezuru kambi ya wakimbizi ya Dadaab kaskazini mashariki mwa Kenya ambapo atasherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Malala alizaliwa 12 Julai 1997 eneo la Mingora, Pakistan katika bonde la Swat.
Alihudhuria shule iliyoanzishwa na babake Ziauddin Yousafzai na baada ya wanamgambo wa Taliban kuanza kushambulia shule za wasichana Swat, alitoa hotuba Peshawar, Pakistan akishutumu Taliban kwa kumnyima wasichana haki ya msingi.
Akiwa na umri wa miaka 14, yeye na familia wake walifahamu kwamba Taliban walikuwa wametoa vitisho kwamba wangemuua.
Tarehe 9 Oktoba, 2012, akirejea nyumbani kutoka shuleni, akiwa kwenye basi, mtu mwenye silaha alimpiga risasi kichwani.
Alipelekwa Birmingham, Uingereza ambapo alipokea matibabu na Machi 2013 akaanza kwenda shuleni.
Mwaka huo pia, aliandika kitabu kuhusu maisha yake.
Aliteuliwa kushindania tuzo ya amani ya Nobel 2013 lakini hakushinda. Aliteuliwa tena 2014 na akashinda kwa pamoja na mwanaharakati mwingine Kailash Satyarthi.
Alikuwa na umri wa miaka 17 na ndiye mtu wa umri mdogo zaidi kuwahi kushinda tuzo hiyo.
Amekuwa akitetea haki za watoto na wanawake.
Post a Comment