Waziri Mkuuwa Israel benjamin Netanyahu anakamilisha ziara yake barani Afrika Alhamisi nchini Ethiopia ambapo anatarajiwa kukutana na viongozi wa serikali na kutia saini mikataba kadhaa ya maendeleo. Tangu kuwasili kwake barani Afrika Julai 4, Netanyahu amezuru Uganda, Kenya na Rwanda katika kile alichokitaja kama histori kubwa kwa Israel kurejea barani Afrika. Amekuwa Waziri mkuu wa kwanza wa Israel kuzuru Afrika katika kipindi cha miaka thelathini.
Ethiopia ilikuwa mojawapo ya nchi za kwanza barani Afrika kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel katika miaka ya sitini. Lakini uhusiano huo umeyumba yumba mara kadhaa baada ya Ethiopia kuukatiza mara kadhaa katika historia yake.
Hii ilidhihirishwa zaidi wakati wa vita vya Waarabu na Israel mwaka 1973 wakati Ethiopia iliposimama pamoja na mataifa mengine ishirini ya Afrika; kukatiza uhusiano kidiplomasia na Israel. Hata hivyo maaptanao yaliafikiwa tena katika miaka ya 1980 baada ya Israel na Misri saini mkataba wa amani mwaka 1979.
Hata hivyo, katika mwaka 1984 Ethiopia ilipokuwa ikikabiliwa na kiangazi na migogoro ya kisiasa wakati wa utawala wa Mengistu Haile Mariam, Israel ilihofia usalama wa maelfu ya Wayahudi wa Ethiopia na kuwaondoa elfu saba kati yao katika safari za siri za ndege katika kile kilijulikana kama kama Operation Moses. Shuguli hiyo iliisababishia Ethiopia aibu kubwa huku awali ikidai kwamba walikuwa wametekwa nyara. Miaka sita baadaye, wengine elfu kumi na nne zaidi walisafirishwa hadi Israeli katika siku mbili tu. Sasa kuna zaidi ya Wayahudi mia moja na thelathini elfu kutoka Ethiopia wanaoishi nchini Israeli.
Hatima ya wengine elfu tisa ambao bado wako Ethiopia inatarajiwa kuangaziwa katika mazungumzo kati ya serikali hizo mbili baadaye Alhamisi. Licha ya hayo, nchi hizo mbili zinajivunia kuwa washirika wa karibu katika vita vya kimataifa dhidi ya ugaidi na kuwa na msaada wa Marekani. Ziara pia anatarajiwa kuendeleza mahusiano baina ya nchi hasa katika maeneo ya biashara, usalama, kilimo na elimu.
Post a Comment