0
TP Mazembe wameendelea mbele katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kupata goli la ugenini dhidi ya Stade Gabesien.
Ilikuwa baada ya matokeo ya mchezo wa mwisho kuisha kwa jumla ya magoli 2-2.
Mazembe Mabingwa wa Afrika,waliingia katika mchezo wa pili siku ya jumanne huku wakiwa nyuma kwa 2-1 mjini Gabes kutokea kwenye mchezo wake wa mwanza na ushindi wa goli 1-0 ukaifanya kusonga mbele.
Mazembe waliingia katika michuano hii baada ya kutolewa katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika na Wydad Casablanca ya Morocco. Michezo mingine itapigwa leo hii ambapo Mabingwa wa Tanzania Yanga watakuwa ugenini kwa faida ya magoli mawili ya nyumbani kukipiga dhidi ya Sagrada Esperanca, Mounana watacheza na Etoile du Sahel huku Medeama wakipepetana na Mamelodi Sundowns ya Afrika kusini.Misr Elmaqasah kutoka Misri watacheza na Al Ahly Tripoli ya Libya huku Kawkab Marrakech wakiwakaribisha Al Merreikh na baadaye FUS Rabat ya Morocco wakikipiga dhidi ya Stade Malien kutoka Mali

Post a Comment

 
Top