0
Afisa wa juu wa umoja wa mataifa wamesema kuwa takriban watu million saba na nusu wanakabiliwa na uhaba wa chakula na kukaribia kukumbwa na janga la njaa.
Uhaba huo wa chakula ni kufuatia mapigano yanayoendelea katika taifa hilo.
Akizungumza baada ya kuitembelea Yemen,John Ging amesema kuwa kuna kiwango kikubwa cha kupungua kwa misaada ya kibinadamu huku mamilion ya raia wa Yemen wakihitaji msaada wa chakula,maji safi na afya. Amesema kuwa kiasi cha billion 1.8 
kilichoombwa na umoja wa mataifa kwaajili ya Yemen ni asilimia 16 pekee ndiyo iliyotolewa. Hivi karibuni serikali ya Yemen ilijitoa katika mazungumzo ya Amani na kundi la waasi wa Shia Houthi baada ya majumaa kadhaa ya mazungumzo yaliyopiga hatua kwa sehemu

Post a Comment

 
Top