Mgombea urais wa chama cha Democratic nchini Marekani Hillary Clinton amejitangaza mshindi kwenye mchujo wa chama hicho katika jimbo la Kentucky.
Huku kura nyingi zikiwa zimehesabiwa katika jimbo hilo, na uongozi wake ukiwa chini ya 0.5%, Bi Clinton ametangazwa kuwa mshindi asiye rasmi na mmoja wa maafisa katika jimbo hilo.
Katika jimbo jingine la Oregon, ambalo pia lilifanya mchujo Jumanne, Seneta Bernie Sanders ameibuka mshindi.
Bi Clinton, ambaye anaongoza kwa wajumbe katika chama cha Democratic, ana matumaini makubwa ya kupata uteuzi Julai.
Alison Lundergan Grimes, mwenyekiti wa bodi ya uchaguzi ya Kentucky, ameambia CNN kwamba matokeo yasiyo rasmi yanaonesha Clinton atapata ushindi mwembamba katika mchujo Kentucky.
Muda mfupi baadaye, Bi Clinton ameandika kwenye Twitter: "Tumeshinda Kentucky! Nawashukuru sana nyote mliojitokeza. Tuna nguvu zaidi daima tukiwa na umoja.”
Bw Sanders, akihutubia mkutano California Jumanne, alisema bado ataendelea na kampeni yake.
Katika chama cha Republican, Donald Trump ameshinda mchujo, jambo ambalo si la kushangaza kwani ndiye pekee aliyesalia kwenye kinyang’anyiro
Post a Comment