Polisi India wamesema kuwa kijana mmoja amejipiga risasi kichwani kimakosa,akitafuta mbinu ya kujipiga picha ya ''selfie'' ya kipekee akiwa na bastola ya babake.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 15 anaendelea kupokea matibabu katika hospitali kuu ya Pathankot iliyoko katika jimbo la Punjab
Yamkini ajali hiyo ilitokea ijumaa jioni kijana huyo aliporejea nyumbani akitoka shuleni .
Walioshuhudia wanasema kuwa alichukua bastola ya babake iliyoidhinishwa na serikali lakini kwa bahati mbaya akajipiga risasi kichwani akitaka kupiga selfie akiwa ameshika bastola kichwani.
Tukio hilo limevutia hisia kali miongoni mwa wenyeji ambao bado wanaomboleza kifo cha kijana mwengine aliyekanyagwa na treni akijaribu kupiga selfie kwenye reli huku gari moshi likija kwa kasi.
Takriban nusu ya idadi ya vifo vya watu 27 vilivyotokea kote duniani mwaka wa 2015 kutokana na picha za ''selfie'' vimetokea nchini India.
Post a Comment