0
Riyad Mahrez amepigwa marufuku kuendesha gari kwa muda wa miezi sita kwa kosa la gari yake kuhusika katika ajali, ingawa mchezaji huyo hakuwa mahakamani wakati kesi yake ikisomwa.
Mchezaji huyo wa timu ya Leicester City, Riyad Mahrez,alihukumiwa wiki hii pia kwa kushindwa kupeleka maelezo yake kwenye kituo cha polisi cha Northamptonshire mnamo October 16 mwaka wa jana kufuatia gari yake aina ya Mercedes Benz kuhusika katika ajali mnamo May mwaka huo.
Mahrez alipigwa faini ya paundi za Uingereza mia tisa na leseni yake kuongezewa makosa na mahakama ya Northampton .
Ambapo mahakama ilimuamuru mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 mbaye hakuhudhuria mahakamani wakati hukumu hiyo ilipokuwa ikitolewa lakini pia kulipa paundi 15 kwa kosa hilo,na paundi 90 kama fidia kwa muathirika wa ajali hiyo.
Polisi wamesema kwamba ,mchezaji huyo anayeishi Leicester, alishindwa kuitikia wito mara tatu wa kuwataarifu nani alikuwa anaendesha gari lake siku ya tukio baada ya kutuhumiwa kuendeshwa kwa kasi kubwa .
Image copyrightP
Katika kandanda uwanjani Mahrez ni mmoja wa wachezaji mahiri uwanjani na mfungaji bora wa mabao msimu huu . Katikati ya wiki hii Mahrez alichaguliwa yeye pamoja na mchezaji mweziwe wa Leicester Jamie Vardy na mwingine ni N'Golo Kante,kuwania tuzo ya mchezajii bora wa mwaka.
Image copyright

Post a Comment

 
Top