0
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis leo anatarajiwa kutangaza wazi msimamo wake kuhusu ndoa, njia za kupanga uzazi na malezi ya watoto.
Tangazo hilo linatarajiwa kuwa kwenye ripoti ya mikutano miwili mikuu ya kutoa maamuzi kuhusu sera za kanisa hilo, maarufu kama sinodi.
Wengi wanatumai kwamba ripoti hiyo itafungua njia kwa kanisa hilo kutoa sakramenti ya komunyo kwa watu waliopewa talaka na wale waliooa tena, jambo ambalo wahafidhina katika kanisa hilo wamekuwa wakipinga.
Ripoti hiyo ni matokeo ya kazi aliyoifanya Papa huyo kwa miaka mitatu.
Mwandishi wa BBC anayeangazia masuala ya kidini Caroline Wyatt anasema ripoti hiyo ambayo kwa Kiingereza hujulikana kama Apostolic Exhortation (Ujumbe wa Papa kwa Waumini) ni nyaraka yenye zaidi ya kurasa 200.
Ripoti hiyo ya sasa imepewa kichwa The JoyPapa Francis alituma hojaji kwa familia maeneo mbalimbali ya dunia akiwaomba wamjulishe matumaini yao na wasiwasi wao.
Baadaye, aliwaita maaskofu na makadinali kwa mikutano miwili ya sera za kanisa mjini Roma.
Kwenye mkutano huo, aliwahimiza kujadiliana na hata kutofautiana kuhusu masuala ambayo hugawanya waumini wa kanisa hilo katika nchi nyingi.
Masuala hayo ni pamoja na kutoa komunyo kwa watu waliopewa talaka na wale walioolewa tena, njia za kupanga uzazi na pia Wakatoliki ambao ni wapenzi wa jinsia moja.
Mwandishi wetu anasema ripoti hiyo itaonyesha wazi msimamo wa Papa Francis.
Baadhi tayari wanasema itashangaza wengi, huku Papa akijitosa katika bahari ya mafundisho ya kanisa Katoliki kuhusu familia.
Wahafidhina hawamtaki abadilishe imani na msimamo wa kanisa, lakini watu wenye msimamo huru wanatumai kwamba ataliambia kanisa liwe na huruma na kuwakumbatia wale watu walio kwenye familia wasiokumbatia kikamilifu mafundisho ya kanisa.
Baadhi katika kanisa Katoliki wametoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua za kumruhusu padri au askofu kuamua faraghani kwa kuzingatia uzito wa kila kisa, iwapo Mkristo aliyepewa au kupeana talaka na kuoa au kuolewa tena anaweza kukumbatiwa kwenye kanisa na kuruhusiwa kupokea komunyo.
 of Love (Furaha ya Upendo)Ingawa wale wanaotaka kanisa likumbatie mambo ya kisasa kama vile Kadinali Walter Kasper wa Ujerumani wanaunga mkono sera hii, wahafidhina wanasisitiza kwamba itadunisha uzito wa msingi uliowekwa na Yesu kwamba ndoa haiwezi ikavunjwa.
Wakati wa kumalizika kwa sinodi ya mwaka jana, Papa Francis aliwakosoa viongozi wa kanisa aliosema wamelifumbia macho suala hilo na kusema kwamba kuendelea kusisitiza kuheshimiwa kwa mafundisho ya dini kikamilifu ni kukosa kutilia maanani dhiki wanayopitia watu wengine katika familia.
Nyaraka hiyo ya papa inatarajiwa kutoa wito wa kuwepo kwa maandalizi mema zaidi kabla ya ndoa na pia kusisitiza mtazamo wa sinodi kwamba ndoa za wapenzi wa jinsia moja haziwezi zikawekwa kwenye kiwango sawa na ndoa za watu wa jinsia tofauti

Post a Comment

 
Top