0
Wakati Watanzania wakikumbuka kifo cha aliyekuwa waziri Mkuu wa awamu ya kwanza, Hayati Edward Moringe Sokoine aliyefariki dunia katika ajali ya gari mkoani Morogoro. Wananchi wameendelea kumkumbuka huku wakiufananisha utendaji kazi wake na wa Rais wa sasa wa awamu ya tano Dr. Johm Magufuli.

Ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya kifo chake, huku mjadala wa utendaji kazi wa Rais Dr. John Magufuli  ukifananishwa na wa waziri mkuu huyo wa zamani, Hayati Edward Sokoine, Startv ikazungumza na mmoja wa mawaziri wa zamani Balozi Ally Mchumo aliyefanya kazi na Sokoine katika baraza la mawaziri wa awamu ya kwanza.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Kampeni na Uchaguzi wa NCCR Mageuzi, Faustin Sungura anasema si sahihi kuwafananisha Sokoine na Magufuli  lakini anaukubali utendaji wa Rais Magufuli kama anavyofafanua.

Balozi Mchumo anaenda mbali za zaidi na kubainisha sababu ambazo zimemfanya Edward Sokoine aendelee kuishi kwenye fikra za Watanzania walio wengi.

Edward Sokoine alipoteza maisha April 12 1984 wakati akitokea bungeni mjini Dodoma akiwa amehutubia kwa mara ya mwisho Aprili 11, 1984 ambapo alikuwa amewataka wabunge kuhakikisha kuwa bajeti itakayowakilishwa iwe imezingatia mambo muhimu ya maendeleao ya wananchi.

Post a Comment

 
Top