0
Ibada maalum imeendelea leo huko Korea Kusini kuadhimisha miaka miwili ya kuwapoteza watu mia tatu wa taifa hilo ambapo wengi kati ya hao wana funzi, ambao walikufa kutokana maafa kivukoni.
Ndugu waliokuwa wakiomboleza walionekana wakirusha maua baharini karibu na mahali ambapo kivuko cha Sewol kilipunduka.
Kikosi cha uokozi kinajiandaa kukiibua kivuko hicho ili kuweza kupata miili ya watu wengine tisa ambao bado hawajapatikana. Wakati kivuko hicho kikizama,inasemekana kilikuwa kimebeba uzito uliozidi uwezo wake kisheria.
Nahodha wa kivuko hicho tayari anatumikai kifungo cha maisha gerezani kwa kosa la mauaji kizembe.

Post a Comment

 
Top