Hadi dola milioni 800 fedha taslimu zinazodhibitiwa na kundi la wapiganaji la Islamic State zimeharibiwa katika mashambulizi ya angani, afisa mmoja wa jeshi la Marekani amesema.
Meja Jenerali Peter Gersten ambaye amepiga kambi nchini Baghdad amesema kuwa Marekani imeripoti kuyalenga maghala yanayoweka fedha hizo.
Pigo hilo kwa IS limesababisha kutoroka kwa wapiganaji wake huku idadi ya wale wanaojiunga na kundi hilo pia ikipungua.
Mwaka 2014 ,idara ya fedha nchini Marekani ilisema kuwa kundi la Islamic State ndilo linalofadhiliwa sana duniani.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Gersten ambaye ni naibu kamanda wa operesheni na intelijensia katika kikosi cha Marekani,amesema kuwa takriban makombora 20 ya angani yaliolenga maghala ya fedha ya kundi hilo yamerushwa.
Hatahivyo hakuelezea vile Marekani ilivyogundua ni pesa ngapi zilizoharibiwa.
Katika kisa kimoja amesema kuwa takriban dola milioni 150 ziliharibiwa katika nyumba moja mjini Mosul nchini Iraq.
Post a Comment