0
Ada ya kupiga simu kupitia mitandao mingine katika muungano wa bara Ulaya imeshuka kwa kiwango kikubwa, ikiwa ni hatua ya mwisho kabla ya ada hiyo kuondolewa kabisa kwa raia wa bara Ulaya mwaka ujao.
Ada hiyo huwa haiwapendezi raia wengi wa bara hilo wanaosafiri kwa shughuli za kibiashara na burudani.
Tume ya muungano huo inasema ada hiyo imeshuka kwa asilimia 75.
Image copyrightGetty
Image captionRaia wa Ulaya anayepiga simu
Serikali imesema kuwa wale wanaopiga simu ,kupakua data ama kutuma ujumbe watahifadhi mamilioni ya pauni kwa ada kufuatia mabadiliko hayo.
Mamilioni ya Waingereza hutumia pauni milioni 350 kila mwaka kutokana na ada hizo za kupiga simu miongoni mwa mataifa ya bara hilo,alisema waziri wa uchumi wa kidijitali Ed Vaizey

Post a Comment

 
Top