0
Rais mstaafu wa Nigeria Goodluck Jonathan amesema kuwa waasi wa Niger Delta wanataka kumuangamiza.
Kupitia kwa taarifa iliyochapishwa na msemaji wake rais Jonathan anasema kuwa madai ya kuwa ndiye anayewafadhili waasi wa Niger Delta Avengers ambao wameshambulia muundo msingi wa uchimbaji mafuta katika eneo lao katika siku za hivi punde.
Wapinzani wake wanadai kuwa rais huyo aliyeondoka madarakani mwaka uliopita huenda anapanga njama na waasi hao ilikuihujumu serikali iliyoko sasa.
Taarifa hiyo inasema kuwa madai hayo yote ni ya porojo.
''Mimi mwenyewe nimelengwa katika mashambulizi kadha yanayolenga kuniua haswa na kundi la Mend (Movement for the Emancipation of Niger Delta )
''sio ukweli kuwa wale waliotaka kuniua sasa ndio wandani wangu''Mimi mwenyewe nimelengwa katika mashambulizi kadha yanayolenga kuniua haswa na kundi la Mend (Movement for the Emancipation of Niger Delta )
Waasi hao wa Niger Delta Avengers wametatiza kabisa shughuli ya uchimbaji mafuta kwa mashambulio ya mara kwa mara kwenye muundo msingi wa mafuta katika jimbo la Niger Delta.
Waasi wa Niger Delta Avengers ambao wameshambulia
Image captionWaasi wa Niger Delta Avengers ambao wameshambulia muundo msingi wa uchimbaji mafuta Nigeria
Wanasiasa na wapiganiaji haki za wenyeji wa eneo la mdomo wa mto Niger, wamelalamika kuwa jamii za Niger Delta, zinastahiki kupewa utajiri unaotoka eneo lao, na wanataka uchafu kutoka visima vya mafuta, usafishwe.
Majuzi tu rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, aliahidi kuwa ataendelea na mpango wa kuwasamehe wapiganaji walioshiriki uhasama dhidi ya serikali.

Post a Comment

 
Top