0
Mchezaji wa mpira wa kikapu nchini New Zealand Akil Mitchell amesema anapata nafuu baada ya jicho lake kutoka alipokuwa uwanjani akicheza.
Mitchell huchezea klabu ya New Zealand Breakers, na alikuwa mjini Auckland kucheza mechi ya NBL ya Australia Alhamisi usiku kisa hicho kilipotokea.
Mchezaji wa timu pinzani aliingiza kimakosa kidole ndani ya tundu la kishimo cha jicho na ghafla jicho lake likatoka nje.
Mchezaji huyo mzaliwa wa Marekani alianguka sakafuni akiwa ametumia mikono yake kufunika jicho lake la kushoto na akakimbizwa hospitalini.
"Kwa viganja vya mkono wangu, nilihisi mboni ya jicho ikiwa nje na kukaa upande mmoja wa uso," aliambia Radio Sport ya New Zealand.
"Bado jicho hilo lilikuwa linaona."
"Nakumbuka nikifikiria, bwana we ... hii ni hali mbaya, lakini nilihisi kwamba lilikuwa jambo la kushangaza na hapo ndipo niliingiwa na wasiwasi kiasi."
JANUARI 26: Akil Mitchell Auckland, New Zealand.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
JANUARY 26: Akil MitchellHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mchezaji huyo wa miaka 24 anasema anakumbuka kusikia mashabiki na wachezaji wake wakiingiwa na wasiwasi.
Alidhani hangeweza kuona tena na kwamba uchezaji wake ulikuwa umefikia kikomo.
"Nilipoingizwa kwenye gari la kubeba wagonjwa walinipa dawa za kupunguza maumivu na matoneo kadha ya dawa yenye chumvi machoni na nikasakia mboni ya jicho ikirudi ndani, jambo ambalo pia lilikuwa la ajabu."
Tweet saying Haki miliki ya picha@AJMITCHELL25/TWITTER
"Najihisi mwenye furaha sana kuweza kufunga na kufungua macho tena, ni jambo la kushangaza."
Baada ya kuruhusiwa kuondoka hospitalini Alhamisi, aliandika kwenye Twitter kwamba "najihisi vyema" na akatumia picha za vibonzo maarufu kama emoji za mboni za jicho.
Mchezaji huyo kutoka jimbo la North Carolina, Marekani anatarajiwa kupona kabisa na huenda akarejea uwanjani kucheza hivi karibuni.

Post a Comment

 
Top