Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari amesafiri kwenda Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo, katika jimbo la Zamfara ili kutangaza kuanza kwa operesheni kubwa ya kijeshi dhidi ya wezi wa mifugo.
Mamia ya watu wameuwawa mwaka huu, huu maelfu wakitoroka makwao kutokana na kukithiri kwa wizi wa mifugo.
Kama kampeini yake ya miezi sita, jeshi la nchi hiyo linatarajiwa kusaka msitu mkubwa mahala ambapo wezi hao wa ngombe wanaaminika kuendeshea shughuli zao .
Kuna hofu kuwa wapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko Haram wamejiunga na magenge hayo ya wizi wa mifugo baada ya kufurushwa kutoka katika ngome yao Kaskazini Mashariki mwa taifa hilo.
Hivi majuzi, shambulizi linalokisiwa kutekelezwa na wavamizi kutoka jamii ya Fulani ilisababisha vifo vya watu 15 katika jimbo hilo.
Mwaka wa 2014 watu 100 waliuawa katika eneo la Maru.
Rais Buahari amekabiliwa na tuhuma za kushindwa kutekeleza ahadi zake wakati wa uchaguzi uliopita ambapo moja ya vibwagizo vyake ilikuwa ni kurejesha usalama kote nchini Nigeria.
Kwa sasa Buhari anakabiliwa na changamoto la mashambulizi ya Boko Haram , wizi wa mifugo na sasa kundi la waasi la Niger Delta ambalo limeahidi kuharibu kabisa miundo mbinu ya usafirishaji wa mafuta kutoka eneo lao hadi mstakabali mpya wa ugavi wa faida itokanayo na mafuta itakaposuluhishwa.
Maelfu ya wakaazi wa eneo hilo la msitu wa Zamfara wametoroka makwao na kuelekea katika majimbo jirani ya Katsina, Kaduna, Niger na Kano.
Wenyeji hao wanalalamikia ukosefu wa usalama.
Post a Comment