0
Seneta wa Vermont Bernie Sanders, ambaye amekuwa aking’ang’ania tiketi ya kuwania urais kupitia chama cha Democratic nchini Marekani amemuidhinisha Hillary Clinton kuwa mgombea wa chama hicho, shirika la habari la Reuters limeripoti.
Bi Clinton na Bw Sanders wamekuwa wakifanya mazungumzo kwa sababu Bi Clinton alikuwa ni kama amehakikishiwa kupata uteuzi tangu mwezi Juni.
Bw Sanders alitumai kuwa na ushawishi kwenye mkutano mkuu wa chama wa kuidhinisha wagombea.
Image copyrightAFP
Lakini wengi wa wafuasi wake wamekuwa wakihama na kumuunga mkono Bi Clinton katika juhudi za kutaka kumzuia mgombea mtarajiwa wa chama cha Republican Donald Trump kushinda uchaguzi wa urais mwezi Novemba.
Bw Sanders alikuwa amesalia kwenye kinyang’anyiro muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa, tangu ibainike kwamba hangepata wajumbe wa kutosha wa kumhakikishia uteuzi wa kuwa mpeperusha bendera wa chama.

Post a Comment

 
Top