0
Michezo ya kutafuta nafasi ya kushiriki Ligi ya Vilabu Ulaya (Europa League) imeanza kuchezwa barani Ulaya kwa michezo 33 kupigwa kwa vilabu 66 vikitafuta nafasi ya kushirki michuano hiyo.
Mtanzania Mbwana Samatta anayekipiga katika klabu ya Genk ya Ubelgiji amefanikiwa kufunga goli la kwanza katika michuano hiyo baada ya kufunga goli la pili katika ushindi wa goli mbili kwa bila ilioupata Genk.
Genk alipata ushindi huo katika uwanja wake wa nyumbani wa Cristal Arena kwa kuifunga Buducnost Podgorica ya Montenegro kwa kuifunga magoli mawili yaliyofungwa na Neeskens Kebano dakika ya 17 na Mbwana Samatta katika dakika ya 79.

Post a Comment

 
Top