0
Matukio ya vitendo vya Ugaidi, Uharamia na madawa ya kulevya yamechangia majukumu ya majeshi ya nchi mbalimbali, kuanza kubadilika.
Hali hiyo pia imechangia kutolewa kwa mafunzo yanayowapa uwezo wanajeshi wa nchi mbalimbali kuweza kupambana na uhalifu huo.
Mafunzo kama hayo kwa sasa yanaendelea nchini Tanzania kwa ushirikiano wa serikali ya nchi hiyo na Jeshi la Marekani na kuzihusisha nchi nyingine za Afrika Mashariki pamoja na Taasisi za Umoja wa Afrika.
Waziri wa Ulinzi wa Tanzania Dokta Hussein Mwinyi amesema matukio ya uharamia ama ugaidi hayana mipaka na hivyo ni lazima yakapigwa vita kwa pamoja, akisisitizia umuhimu wa kuwepo kwa mafunzo kama hayo.
Ushirikiano wa pamoja wa kijeshi pia umechangia kusaidia kumaliza matukio ya uharamia, katika bahari kuu yaliyoathiri nchi jirani ikiwemo Tanzania kutokana na kutokuwepo kwa serikali dhabiti nchini Somalia.
Mafunzo hayo yaliyozinduliwa jana Jumatatu jijini Dar es Salaam pia yanazishiriukisha nchi za Uingereza na Ujerumani pamoja na Shirika la Kimataifa la RedCross.

Post a Comment

 
Top