Mshambulizi wa zamani wa klabu ya Chelsea ya Uingereza Demba Ba amevunjika mguu akiwa uwanjani katika mechi ya ligi kuu ya Uchina.
Raia huyo wa Senegal mwenye umri wa miaka 31 alikabiliwa na mlinzi wa timu hasimu katika ligi kuu ya Uchina hapo jana Jumapili tarehe 17 Julai.
Ba ambaye anaichezea Shanghai Shenhua aligongwa na mchezaji wa timu hasimu ya Shanghai SIPG mita chache tu kabla ya kisanduku cha hatua 18, Alipoanguka mguu wake ulipinduka kwa hali isiyo ya kawaida na kuvunjika papo hapo.
Video ya mechi hiyo inaogofya haswa inavyoonesha wazi wazi mguu wake umevunjika kati ya goti na kisigono.
Kocha wa klabu yake Gregorio Manzano ameonya kuwa tukio hilo linaweza kumlazimisha nyota huyo kustaafu kucheza soka .
lmcheBa aliwahi kuichezea West Ham, Newcastle na Chelsea zote katika ligi kuu ya Uingereza kabla ya kujiunga na klabu hiyo ya Uchina akitokea Uturuki katika klabu cha Besiktas.
Uhamisho huo yamkini uligharimu takriban pauni milioni 12.
Msimu huu Ba anaongoza orodha ya wafungaji mabao akiwa na jumla ya mabao 14 katika mechi 18 alizoshiriki.
Post a Comment