Mwanaharakati nchini India Irom Sharmila anakamilisha mgomo wake wa kukataa chakula dhidi ya sheria tata baada ya miaka 16.
Mwanaharakati huyo anatarajia kuanza kula hii leo baada ya mahakama katika jimbo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo la Manipur kumuachilia huru leo.
Amekua katika mahabusu ya mahakama na kulazimishwa kula kupitia mrija kupitia pua lake kuepuka sheria inayoadhibu uhalifu wa kutaka kujiua.
Lakini mwezi uliopita aliiambia mahakama kwamba anataka kukatiza mgomo wake na kuanza kampeni yake kama mgomea huru katika uchaguzi ujao wa wabunge .
Bi Sharmila amekua akipinga sheria inayopatia jeshi mamlaka maalum (AFSPA), ambayo inawapatia wanajeshi mamlaka yote ya kuwakamata watu bila vibali na hata kupiga risasi kwa lengo la kuua katika majimbo kadhaa nchini India , likiwemo jimbo la Manipur na la Kashmir.
Mpiga picha Ian Thomas Jansen-Lonnquist alifuatilia kwa karibu safari yake katika miaka michache iliyopita.
Alianza mgomo wake wa kukataa chakula miaka 16 iliyopita baada ya raia 10 kuuawa na askari wa India katika mji wa Manipur.
Ameishi kipindi kirefu cha miaka 16 chini ya uangalizi wa mahakama katika hospitali ya ya mji mkuu wa jimbo la Manipur, Imphal,ambako alilazimishwa kunywa mchanganyiko wa madawa na maziwa ya unga ya watoto wachanga
Bi Sharmila aliachiliwa huru mwezi Agosti 2014 baada ya mahakama kukataa shitaka kwamba "anajaribu kukujiua ". Lakini alikamatwa tena siku mbili baadae baada ya kukataa kumaliza mgomo wake.
Bi Sharmila alikuwa akihudhuria mahakama kuu ya Manipur kila baada ya wiki mbili kurejelea msimamo wake mgomo.
Mgomo wake wa chakula ulitambuliwa kote duniani, ambapo shirika la haki za binadamu la Amnesty International lilimuelezea kama mfungwa mwenye mawazo huru.
Mwanaharakati huyo alivivutia vyombo vya habari vya ndani ya nchi na vya kimataifa katika miaka ya hivi karibuni .
Bi Sharmila alikua na ufuasi wa wanawake na makundi yanayopigania haki za kijamii katika jimboni.
Makumbusho yamejengwa katika eneo la Manipur ambako raia 10 waliuliwa na wanajeshi wa India. Jimbo hilo lina jumla ya wakazi milioni 2.5 na kikosi kikubwa cha wanajeshi , na polisi wengi walipelekwa huko kukabiliana na makundi ya waasi.
Post a Comment