Kiungo wa kati wa timu ya Manchester
City Yaya Toure amepiga chini ofa ya dola za kimarekani 459,000 kwa
wiki iliyotangazwa na China.
Toure mwenye umri wa miaka 33 angekuwa mchezaji muhimu katika ligi ya uchina inayotarajiwa kufanyika msimu ujao.Ameamua kupingana huku mkataba wa mchezaji huyo wa Ivory Coast ukitarajiwa kuisha majira ya joto.
Mustakabali wa Toure ulionekana kuwa njia baada ya kuachwa nje ya kikosi tokea mwanzo wa msimu.
Toure amekuwa huru kusaini mkataba mpya na timu yoyote kutoka nje ya Uingereza lakini anakiri kuwa ana furaha kuendelea kubaki EPL.

Post a Comment