0
Kufika sasa Afrika imeshinda medali mbili kupitia waogeleaji wa Afrika Kusini, Chad Le Clos na mwenzake Cameron van der Burgh.
Wote wamepata medali za fedha.
Clos alikuwa wa pili shindano la mita mia mbili mtindo wa freestyle la wanaume, mshindi akiwa ni Sun Yang wa China..
Burgh amefuzu kwa fainali ya mita 200 mtindo wa Butterfly baadaye leo hii anakonuia kutetea taji lake aliloshinda London miaka minne iliyopita lakini anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa nyota wa Marekani Michael Phelps anayelenga kupata dhahabu yake ya 20.
Kwa jumla Afrika Kusini ni ya 21 kwenye msimamo wa medali pamoja na Indonesia na New Zealand.
Timu ya Kenya ya Raga ya wachezaji 7 kila upandeImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionKenya ilishindwa na Uingereza katika mechi ya ufunguzi
Bingwa mtetezi, Marekani inaongoza ikiwa na jumla ya medali 19 ikifuatiwqa na China 13 na Australia ni ya tatu na medali saba.
Kwa upande wa dhahabu Marekani na China wote wana dhahabu tano na Australia dhahabu nne.
Tukiangazia mataifa ya Afrika Mashariki, mabondia wa Kenya wanazidi kunawiri kwani jana Peter Mungai ameanza vyema kwa kumshinda Bin Lv wa China kwa pointi uzani wa light-flyweight.
Bondia mwingine wa Kenya Rayton Okwiri naye pia alishinda pigano lake la kwanza Jumapili uzani wa welter na siku hiyo hiyo Kennedy Katende wa Uganda akashindwa kwa TKO raundi ya kwanza na Joshua Buatsi wa Uingereza uzani wa light-heavy.
Mabondia wa Afrika Mashariki ambao bado hawajacheza ni Ronald Serugo wa Uganda uzani wa 'fly' na Benson Gicharu wa Kenya uzani wa bantam..
Timu ya Kenya ya Raga ya wachezaji 7 kila upandeImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionTimu ya Kenya ya Raga ya wachezaji 7 kila upande
Nigeria inafanya vyema kwenye mchezo wa tenisi ya meza huku Angola ikiwika kwa mpira wa mikono upande wa wanawake kwani kufikia sasa wameshinda mechi zao zote mbili na wako nafasi ya kwanza kundi A pamoja na Brazil. Jumla ya mataifa 206 yanashiriki michezo ya Olympiki ya mwaka huu

Post a Comment

 
Top